Hakuna fataki-vimulimuli tena! - Ministry Magazine Advertisement - Ministry in Motion 728x90
 

Hakuna fataki-vimulimuli tena!

Login
  english / français
Makala / 2018 / May

 

 

Hakuna fataki-vimulimuli tena!

Jacques François

Jacques François, MA, serves as pastor of the New Life Adventist Church, Louisville, Kentucky, United States.

 

Ilionekana jambo lisilowezekana kwangu wakati nikiwa kijana kuficha furaha yangu wakati Julai 4 ilipokaribia kila mwaka. Ari na woga vilishindana tumboni mwangu wakati nilipofikiria juu ya kipindi cha sherehe. Ari kubwa kwa sababu ya milipuko midogo iliyosababishwa na mabomu ya moshi, roketi za chupa, fataki, mishumaa ya kirumi, vilipuzi vinavyorushwa kwa mzinga, na fataki zinazolipuka kwa kurudia rudia. Woga kwa sababu wakati wote nilitumaini kuwa huo ungekuwa mwaka ambao ningefaulu kupanda kutoka kutumia fataki - vimulimuli kwenda fataki zinazotoa sauti zilizokuwa zinapatikana katika ghala la silaha.

Kila mwaka mama yangu alinunua fataki - vimulimuli kwa ajili ya watoto kujifurahisha. Tulipokuwa wadogo sana, kimulimuli kilitosha kabisa kuzima kiu yetu ya starehe. Kadri tulivyokuwa wakubwa, mioyo yetu ilikuwa na shauku ya kile tulichoita “fataki” halisi. Tulimsihi mama yangu kuboresha akiba iliyokuwepo ya vimulimuli ili pawepo aina nyingi zaidi za kutuwezesha kuchagua kile tukipendacho zaidi. Mwaka mmoja hatimaye, alikubali na kununua fataki nyingi kabisa.

Mpwa wangu pamoja nami (tulikuwa kama ndugu kwa vile umri wetu ulilingana) tulifurahia sana maboresho hayo. Tulianza kazi mara moja. Jioni ilianza kwa kuwasha fataki moja baada ya nyingine. Kwa vile barabara yetu ilikuwa imechafuliwa na chupa tupu za bia zilizotupwa kienyeji kando kando, tuliamua kuwashia fataki kwenye chupa ili tuone kama zitalipuka. Tuliridhika kuona zikilipuka. Baada ya kulipua chupa kadhaa tukapata wazo la mwisho. Tuliamua kujaza fataki kwenye chupa na kujaza chupa nyingi kadri ilivyowezekana kwenye sanduku letu la barua. Kisha tukawasha na kufunga mlango wa sanduku letu la barua na kukimbia kwa kasi kadri tulivyoweza. Punde tukasikia mlipuko mkubwa ajabu! Tuliporudi kuangalia lile sanduku lilikuwa limeharibika kabisa. Lilikuwa limetoboka kila mahali, mlango ulirushwa mbali barabarani, na mlipuko ulikuwa mkubwa kiasi kwamba uling’oa sanduku letu la barua la plastiki toka mahali pake.

Kitendo hiki kwa kweli kilikuwa cha hatari sana. Siwezi kueleza hatua alizotuchukulia mama.

Mlipuko wa Injili

Fataki zinalipuka; kadhalika na injili. Injili inasababisha milipuko mikubwa inayoharibu ufalme wa shetani na kutikisa msingi wa uwezo wa dhambi. Katika Warumi 1:16, “Kwa maana siionei haya injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye.”*

Neno “uweza” linatokana na neno la kiyunani dynamis, ambalo ndilo neno mzizi la kiingereza linalomaanisha baruti kali. Mungu ameweka kijiti cha baruti kali mikononi mwetu kufutilia mbali kikwanzo chochote katika kufikia uzima wa milele ambayo adui anaweka katika njia ya binadamu. Mungu anajua kwamba hatuwezi kuleta uangamivu mkubwa wa aina hii kwa kutumia vilipuzi. Kama baruti kali, injili inalipua vitu. Injili inapotolewa, matokeo yake ni jamii ya watu wenye uzoefu wa neema iokoayo ya Mungu. Ngome imara ya dhambi inasambaratishwa, miali ya haki ya Kristo (Warumi 1:17) inawashwa, na urejeshwaji wa sura ya Mungu unapandikizwa katika uumbaji wake.

Pentekoste ilizindua msimu ambao haukuwahi kuwepo wa kuhubiri injili kwa ujasiri. Asubuhi ile kulikuwa na washiriki 120 wakiomba kwa bidii. Baada ya Roho wa Mungu kujimimina kwa kanisa, injili ilihubiriwa kwa ufasaha, na vumbi lilipotulia watu 3000 walikuwa wameongezeka katika vitabu vya kanisa.

Ni lazima niweke wazi kwamba hakuwa Petro pekee aliyehubiri siku ile. Roho Mtakatifu alimwagwa juu ya kila mtu aliyekuwa katika chumba cha juu (Mdo. 2:2,3). Fungu la nne linarudia Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.” Aya ya 11 inapanua dhana hii kwa kusema, “tunawasikia hawa wakisema kwa lugha zetu matendo makuu ya Mungu.”Katika kanisa linalokua, si mhubiri tu anayetangaza injili. Kila mmoja amepewa sanduku la baruti za injili. Injili ililipulika wakati wa Pentekoste, na watu 3,000 walichimbuliwa kutoka katika vifungo vya mauti. Kama ambavyo mimi na mpwa wangu tuliwasha fataki Julai 4 na kuzishindilia katika sanduku la barua la mama yangu, ndivyo watu wa Mungu walivyowasha baruti zao siku ya Pentekoste na kuzishindilia katika lindi kuu la dhambi na likalipuliwa na kuondolewa katika misingi yake.

Lipua

Kila mwaka tulisimama tukipunga fataki-vimulimuli katika mduara hadi pale moto wake ulipozimika kabisa. Hiki kilikuwa kitu cha kupendeza ingawa hakikuwa na manufaa. Mama yangu alitupatia fataki - vimulimuli kwa vile vilikuwa salama na havikuleta madhara yoyote. Fataki kwa upande mwingine zilileta uharibifu wa kutisha kwa sanduku la barua. Nguvu ya ule mlipuko ililifanya lisifae tena kwa matumizi yoyote. Hata hivyo, kuna kitu kilichofanana kwa vimulimuli na fataki. Ingawa vimulimuli na fataki vilitofautiana kimaumbo, ili vyote viweze kutenda kazi vilihitaji kuwashwa kwa moto.

Injili inauwezo wa kulipulia mbali chochote kilicho katika njia yake, lakini inahitaji moto ili ichochoe nguvu yake ya uangamivu. Pasipo mwali wa Roho Mtakatifu kuhubiri injili hakutaleta badiliko lolote.

Ni lazima niseme kwa ujasiri – Injili ilikusudiwa kuhubiriwa! Kama tukitazama agizo kuu la utume wetu, utagundua kuwa sehemu mbili za kwanza mahusus kabisa zinatutaka kuhubiri, wakati ambapo sehemu ya tatu inatutaka kufundisha. Kila Biblia inapojadili mada ya injili, mara zote inafanya kwa muktadha wa kuhubiri. Mungu alikusudia injili iwe ya kuleta mabadiliko, na si ya kutaarifu tu.

Nilipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Florida State(FSU), wanafunzi wote walipewa tiketi za bure kuhudhuria mechi za nyumbani za mpira wa miguu. Uhalisia kwangu ulikuwa tofauti kiasi cha kutisha darasani ukilinganisha na kwenye mechi ya mpira. Darasani niliketi nikasikiliza na kunakili kile alichosema mkufunzi,na kutumia fursa hiyo kuuliza swali pale ambapo sikuelewa. Mawasiliano kati yangu na mwalimu yalikuwa na mpangilio, mipaka, na yaliyokusudiwa kunifundisha kitu ambacho sikuwa nimewahi kukifahamu. Hata hivyo, kwenye mechi ya mpira wa miguu hisia zangu ziliendana zaidi na matokeo ya mechi. Pale FSU ilipozidiwa, ikawa nyuma kimagoli, na hatimaye ikapoteza mechi, nilijawa wasiwasi, nilijisikia vibaya sana, mkali, na mwenye huzuni sana. Timu yangu ilipofanya vizuri na tukashinda, hisia na mwonekano wangu vilibadilika kabisa. Nilikuwa na furaha, nilihemewa na furaha, na kouna fahari sana. Ungefurahi kusikia mvumo wa sauti zetu tukishangilia timu yetu. Darasani nilijishughulisha kiakili na masomo yangu. Katika mechi ya mpira wa miguu, Nilijishughulisha kimajaribio na matokeo ya mechi. Si nia yangu kuhimiza hali ya kuhemkwa mno. Napendekeza kuwa kuhubiri humpa fursa msikilizaji kupata uzoefu wa habari njema za Yesu Kristo.

Neno la Kiyunani la “injili” ni euangelion nalo linafasiriwa kama “habari njema” au “injili” ingawa historia yake ni kubwa. Wakati wafalme walipoenda katika uwanja wa vita, wajumbe waliotumwa walileta habari kwa wananchi juu ya matokeo ya vita. Walinzi walisimama juu ya kuta za jiji wakingoja habari toka kwa mjumbe. Mjumbe aliukaribia mji kwa mwonekano mahsus ambao uliashiria kuwa mfalme ameshinda au ameshindwa. Kama mwonekano wa mjumbe uliashiria kuwa mfalme ameshinda, mlinzi alipaza sauti yake akisema: “Eungelion! Mfalme wetu ameshinda.” Wakazi wa jiji walikuwa katika hali ya hatari kihisia. Ikiwa mfalme wao angeshindwa, wangefanywa watumwa au kuangamizwa na mfalme mpinzani. Wanachi walishangilia kama ambavyo wangefanya iwapo wangekuwa vitani na jeshi la mfalme wao. Ukweli kwamba mfalme wetu ameshinda vita unapaswa kutufanya tushangilie kuliko ambavyo tungefanya katika mechi ya mpira wa miguu na kuona timu yetu ikiwasambaratisha wapinzani wake.

Inayostahiki

“Roho wa Bwana yu juu yangu,

Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema.

Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao,

Na vipofu kupata kuona tena,

Kuwaacha huru waliosetwa,

Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.” (Luka 4:18, 19) 

Tunapochunguza huduma ya Kristo, ni rahisi kugundua kipengele cha utabibu wa miujiza yake. Alikuwa tabibu wa tiba ya ngozi, kwa vile alirejesha wororo wa ngozi kwa wenye ukoma. Alikuwa tabibu wa macho, kwa vile alirejesha maono kwa wasioona. Alikuwa tabibu wa damu, kwa vile alimponya mwanamke aliyekuwa akitokwa damu. Alikuwa tabibu wa mifupa na misuli, kwa vile alimponya aliyepooza. Kwa mujibu wa aya hii Kristo alitiwa mafuta kuhubiri, na injili ilistahiki kushughulikia nyanja za kiroho, kijamii, na nyanja ya kihisia ya hali ya mwanadamu pia. Mungu aliipatia injili pia kuponya mioyo iliyovunjika, kuwapa uhuru waliotekwa na wanaoteseka, kuponya upofu wa kiroho na kuleta tumaini kwa ajili ya siku za usoni. Injili inatengeneza njia kuu kwa ajili ya wokovu.

Hii ndiyo sababu hasa ya injili kuwa baruti kali: kwa vile inalipukia kwenye miamba na maumbo mbambali yanayokwamisha maendeleo ya mdhambi katika kubadilishwa. Ina faida gani baruti kama hakuna moto wa kuiwasha? Injili ina faida gani kama hakuna mhubiri wa kuiungurumisha toka vilele vya milima? Mlipuko wa injili unapowaka unawasha baruti ya injili na kutupilia mbali vikwazo vyote vilivyo katika njia ya wokovu wa mwanadamu.

Paulo katika waraka wake kwa Warumi anasema,” Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa,

Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!”(Rum. 10:14, 15)

Injili huzungumza kwa njia ya kuhubiri. Sehemu ya aya inayotangulia inatupatia vipengele vinavyofuatana kimoja baada ya kingine. Kipengele tangulizi ni mhubiri aliyejazwa Roho Mtakatifu! Wakati nasoma shahada ya uzamili katika masomo ya uchungaji, mmoja wa maprofesa wangu aliuliza swali darasani? Injili inapataje usikivu? Yawezekana nina rahisisha mno jibu lake, lakini kulingana na Warumi 10:14 ni kwa njia ya kuhubiri.

Kwa mujibu wa Maandiko, “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri” (Mt. 3:1); “Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu,” (Mk. 1:14); Wanafunzi “wakahubiri kotekote” (Mk. 16:20); mitume “kuhubiri katika Yesu ufufuo wa wafu” (Mdo. 4:2); na Yesu alituambia katika agizo la injili kuhubiri (Mk. 16:15; Luka 24:47).

Si Mchungaji Peke Yake

Uelewa potovu mbaya na mkubwa kabisa uliomo ndani ya mwili wa Kristo ni kwamba agizo la injili linaweza kutimizwa kupitia maneno na nguvu za mchungaji peke yake. Mimbari ni zana kuu ya mchungaji, lakini mimbari isichukuliwe kuwa kizimba cha injili. Mungu alikusudia injili ipenye kupitia njia kuu na ndogo, barabara na vilele vya milima.

Hebu pitia kitabu cha Matendo pale ambapo kusanyiko la maombi linahimiza kuomba sura ya 1 aya za 13-15. Watu 120 wamo chumba cha juu wakiomba na kupeleka dua zao. Wakati sauti ya mvumo, upepo wenye nguvu ulipojaza nyumba walimokuwa wakiomba, ndimi za moto zikawakalia kila mmoja wao katika Matendo 2:3 . Aya ya 4 inaendeleza hoja kwamba wote walijawa na Roho Mtakatifu, na wakaanza kunena kwa lugha zingine kadri Roho alivyowajalia kunena. Katika aya za 8 na 11 kila mtu akasikia matendo ya ajabu ya Mungu katika lugha zao. Mpaka hapa Petro hajasimama kuhubiri. Injili ilihubiriwa na kila mtu aliyejazwa na Roho wa Mungu.

Ruhusu fikra yako takatifu kupiga picha kidogo pale ambapo kila mshiriki katika kanisa lako atakapotoka kwenda kutafuta kundi la watu katika jamii na kuanza kuhubiri matendo ya ajabu ya Mungu kwa wakazi hao. Na kwamba kazi ya mchungaji ibakie kutoa wito mimbarani kama Petro alivyofanya na kuwataka watu kutubu, na kubatizwa kwa jina la Yesu Kristo, kupokea ondoleo la dhambi, na kupokea karama ya Roho Mtakatifu (Mdo. 2:28). Piga picha ya aina ya nguvu na joto litakaloletwa na huku kuhubiri injili na matokeo yake kwa jamii. Je kingekuwa kitu cha namna gani kuzifikia kona zote za mji, majengo makubwa, ujirani, majiji, nchi, na mabara kwa ajili ya Kristo kupitia namna zake za makusudi na madhubuti za uinjilisti?

Ulimwengu hauhitaji mtaaalamu mwingine wa ustadi ya kuhubiri au mwanateolojia. Ulimwengu unashauku kubwa na watu jasiri wasioogopa kufungua midomo yao na kutangaza habari njema ya Yesu Kristo! Mungu anataka kila mtu ashiriki kutimiza agizo kuu kabisa kupata kutolewa kwa jamii ya wanadamu. Maana ya msingi kabisa ya kuhubiri ni kutangaza. Kila mmoja, hata bila elimu ya teolojia, anaweza kutangaza habari njema za Yesu. Muulizae mkoma wa Galilaya (Mk. 1:40-45), mmoja wa wakoma kumi aliyeponywa kati ya Samaria na Galilaya (Luka 17:11–19), mtu aliyeponywa kando ya dimbwi la Bethsaida (Yn. 5:2–15), na mwanamke kisimani (Yohana 4). Sharti moja lilitangulia kuhubiri injili katika visa hivyo: kila mmoja wao alikuwa amepata uzoefu wa wema wa Yesu Kristo.

Chagua sehemu ya jamii na uishambulie na jeshi lako la waumini kama wale 120 walivyofanya siku ya Pentekoste. Peleka kila mshiriki kutangaza injili kwa kila mtu wanaye kutana naye katika jamii. Tangaza injili toka nyumba hata nyumba na kutoka jumba linalokaliwa na wengi  hadi jumba linalokaliwa na wengi. Tembelea mbuga, sehemu za burudani au mapumziko, na stoo za vinywaji. Ivamie jamii kama dhoruba. Muombe Mungu akupe ujasiri mtakatifu – na uhubiri injili kwani kwa hakika kuna uweza wa Mungu katika kutangaza habari njema.

Advertisement - RevivalandReformation 300x250

Ministry reserves the right to approve, disapprove, and delete comments at our discretion and will not be able to respond to inquiries about these comments. Please ensure that your words are respectful, courteous, and relevant.

comments powered by Disqus

 

back to top