Advertisement - ESDA 728x90
 

Kumtafuta Mungu Asiyeonekana

Login
  english / français
Makala / 2019

 

 

Kumtafuta Mungu Asiyeonekana

W. Floyd Bresee

W. Floyd Bresee, PhD, served as secretary of the General Conference Ministerial Association between 1985 and 1992. He is retired and resides in Santa Rosa, California, United States.

 

 

Fikiria kidogo juu ya binti wa umri wa miaka mitano ambaye tutamwita Maria. Vitu viwili ambavyo Maria anavipenda kuliko vyote ni baba yake na mchezo wake kipenzi, kujificha na kutafutana. Moja ya sababu hasa ya kumpenda baba yake ni kwa vile wakati mwingine hucheza naye mchezo wa kujificha na kutafutana.

Jioni moja Maria anamwomba baba yake wacheza ule mchezo wake. Hatua kwa hatua wanatoka nje kwenda katika uwanda wa nje ya nyumba yao kwa ajili ya mchezo wao mdogo wa kujificha na kutafutana. Maria anajitolea kuanza, anageuka nyuma, anafumba macho yake na kuhesabu mpaka kumi wakati baba yake akijificha. “Nakuja, uko tayari au bado?” Kwa hakika, baba yake amekwisha jificha kama alivyotakiwa- sasa haonekani.

Anatafuta hasa: nyuma ya nyumba ya mbwa, ndani ya nyumba ya mbwa; nyuma ya mti, kuzunguka nyumba ya midoli, ndani yake; nyumba ya chombo cha taka, ndani yake. Anazunguka na kuzunguka. Sasa jua linazama. Giza linaingia, na baba bado haonekani. Huenda ameondoka akamwacha! Anaanza kuwa na wasiwasi. Tabasamu lake linafifia. Machozi yanatoka. Lakini baba, aliyejificha nyuma ya kichaka kikubwa, anaona na kutambua hofu yake. Anajaribu kukohoa kidogo, anatikisa tawi. Maria anasikia, anamwona, na kujawa tabasamu huku akimkimbilia.

Huenda kijana fulani anahangaishwa na mashaka kama kweli yupo Mungu mwenye upendo asiyeonekana. Au mtu wa umri wa kati anakabiliwa na tatizo lisilotatulika na kujiuliza kama Baba asiyeonekana anajali hasa. Au mchungaji mzoefu anaona jioni ya maisha yake inakaribia na anaanza kuhofia siku za usoni. Habari njema ni kwamba kama ilivyoahidiwa na Baba yetu asiyeonekana katika Yeremia 29:13 “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote”

Kumtafuta Mungu ni Muhimu

Kumwamini Mungu ni muhimu katika ulimwengu wetu wa sasa. Yesu aliahidi, “ ‘Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga’ ” (John 14:27).

Tulikusudiwa kule Edeni tufurahie kuwa na Mungu. Hiyo ipo katika vinasaba vyetu. Kuna tundu alilotengeneza Mungu katika moyo wa binadamu ambalo haliwezi kuzibwa na kitu kingine chochote. Ni Mungu tu anayeweza kulijaza hilo, kujazwa na imani yetu kwake. Imani kwa Mungu, kwa hiyo, ni ya muhimu katika ulimwengu wetu wa sasa.

Imani kwa Mungu ndilo tumaini letu pekee kwa ajili ya ulimwengu ujao. Mungu anaahidi katika Yeremia 29:11, “ ‘Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.’”

Wale wanaotafiti juu ya mwenendo wa mwanadamu wanasema kwamba wengi wetu tunatumia yapata asilimia 12 ya siku nzima kufikiria juu ya siku zijazo. Agostino aliisema kwa namna ya kuvutia mno, “Tunadhoofishwa uwezo wetu wa kusikia na kelele za hali ya juu za minyororo ya kifo.” Lakini kifo si neno la mwisho, ni la pili kutoka mwisho, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi”(Yohana 11:25).

Mungu Anapatikana

Mungu anataka apatikane. Ni kwanini baba ya mtoto Maria alijaribu kukohoa na kutikisa lile tawi? Kwa kuwa alimpenda na alitaka kumfanya binti yake aliyekuwa na huzuni pamoja na woga kuwa na furaha tena. Baba yetu wa mbinguni asiyeonekana alitaka kutufanya tuwe na furaha tena, na hivyo akamtuma kwetu Mungu anayeonekana, Yesu aliyesema,”Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha” (Mt. 11:28).

Mungu anapatikana, hata katika umri wetu wa uzee. Aliahidi: “ ‘na hata uzee wenu mimi ndiye, na hata wakati wenu wa mvi nitawachukueni; nimefanya, nami nitachukua; naam, nitachukua na kuokoa.’ ” (Isa. 46:4). Kuchukua kunamaanisha kitu fulani maalumu kwa wazee. Tulipokuwa vijana tulikuwa tunataka kuruka toka mikononi mwa mama zetu ili tufanye mambo yetu wenyewe. Katika umri wa uzee, tunageuka kuhitaji msaada wa ziada tena.  Sasa ni fimbo, gongo, na vyombo vya kutembelea, kiti chenye magurudumu, au mkono wa mtu mwenye nguvu. Mungu kujitolea kutuchukua kwa mkono wake wenye nguvu ni ahadi ya thamani.

Mungu anapatikana kwa wale wamtafutao kwa moyo wote

Fungu la Yeremia ambao tulianza nalo tafakari hii linatuhakikishia kuwa Mungu anapatikana kwa wale wamtafutao kwa moyo wote - ‘Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote’ ” (Jer. 29:13).

Moyo wa baba yake Maria uliguswa na jinsi Maria alivyotafuta kwa moyo wote: mtini, nyumba ya mbwa, nyumba ya midoli, chombo cha taka – tena na tena. Baba yetu wa mbinguni anaguswa na utafutaji wetu kwa moyo wote.

Lakini je saa moja ya ibada kwa juma ni utafutaji kwa moyo wote!!

Mtafutaji mwenye moyo uliogawanyika hawezi kumwona Mungu asiyeonekana. Kinyume chake ni kwamba si kwamba tu mtu mwenye moyo uliogawanyika hatampata Mungu – bali kwa vile utafutaji wao wa kienyeji haumpati Mungu, wanaishia kumlaumu kuwa hapatikani!

Kwa maneno mengine fungu letu la Yeremia linasema, “Mtakapokuwa makini na bila mzaha katika kunitafuta na kunihitaji zaidi ya kitu kingine chochote, nitahakikisha kwa hamuishii katika masikitiko” Uhakika ulio heri kiasi gani!

Mungu anapatikana kwa wamtafutao kila siku kwa moyo wote

Kumbuka kanuni ya bidii, isemayo, “Nguvu zinahitaji marudio.” Jifunze kuitii kanuni hiyo. Kama umewahi kuweka mkono au mguu wako kalibuni au ukalazwa kwa siku kadhaa, utakumbuka jinsi misuli isiyofanya kazi inavyoweza kuishiwa nguvu kwa haraka. Kama hutumii miguu yako isipokuwa kwa kuja kanisani siku moja tu kwa juma, itakoma kufanya kazi. Ili kuwa thabiti misuli yetu ya miguu na ile ya kiroho inahitaji mazoezi ya kila siku.

Kuna sehemu tatu ambazo wamtafutao kila siku kwa moyo wote, waweza kumtafuta Baba asiyeonekana:

1. Kitabu. Vitabu vya kesha ni vya manufaa, lakini haviwezi kuwa bora zaidi ya Biblia! Kama umejaribu mpango wa kusoma Biblia kila siku na ukakuchosha, nakupa changamoto ujaribu njia hii. Tafuta toleo la Biblia ulipendalo, lifungue kila siku, na kwa maombi soma mafungu machache toka Mathayo 5-7. Kama ukifanya hivyo kila siku maisha yako yote, najua utatokea kumjua na kumpenda Mungu asiyeonekana.

2. Maombi. Yeremia 29:11, 12 inasema:“ ‘Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.’ ” Maombi ni njia moja ya kumtafuta Mungu: Ombi lina sehemu tatu:

Shukuru. Mshukuru Mungu kwa hewa unayovuta, moyo wako unaoendele kudunda, na chakula ulacho. Chakula chetu hata hivyo, hakitoki sokoni. Kimsingi kinatokana na mbegu, udongo, jua na maji – na ni Mungu avitoaye vyote hivyo. Chakula ni uthibitisho bayana mno wa Mungu asiyeonekana.

Omba. Ahadi ya Yeremia ni “Utaita . . .omba . . . nami nitasikiliza .” Kwanza omba msamaha wa dhambi. Ndipo baada ya hapo uikumbuke familia, marafiki, na orodha yako ya mambo ya kuombea.

Jitolee. Hii ni sehemu ya ombi iliyosahauliwa kuliko zote. Usiseme tu, “Nitumie mahali fulani.” Hiyo ni njia tu ya kutuliza dhamiri yako. Jitolee kwa kazi mahususi ambayo umeshirikiana na Mungu kuichagua. Atakusaidia kupata kitu kinachowafaa wale na mahali pale ulipo. Ili mradi anakupatia hewa ya kuvuta, atakupatia mahali pa kumtumikia. Hii ndiyo tiba kwa ombi la kibinafsi. Huduma yetu kwa wengine ndivyo upendo wa Baba yetu asiyeonekana unavyoonekana kwa ulimwengu.

3. Asili. Mtu aliyekuwa akitaka kuwa mkanaMungu alimwangalia binti yake akila kwenye kiti chake kirefu. Alimwangalia akijaribu njia kadhaa za kupeleka chakula mdomoni mwenyewe. Alimsikia akibwabwaja katika harakati za kujifunza kuongea. Lakini zaidi ya vyote, alijifunza namna ya masikio yake makamilifu lakini yenye utendaji wa ajabu akasema, “Haiwezekani kwamba haya yote yametokea kwa bahati tu. Lazima kuna Mungu.”

Majusi walitabiri kwa miezi kadhaa kwamba jua, dunia na mwezi kuwa katika mstari mmoja kungesababisha “mwezi kuonekana mwekundu”, ikionekana vyema kabisa juu ya makazi yetu saa 11:30 alfajiri, Januari 31, 2018. Tulitegesha kengele ya saa, na kwa hakika mwezi wote ulionekana mwekundu. Kwangu mimi ilikuwa muda wa kustaajabu. Unaona, Wanadamu hawakuuumba huo mwezi au kuuhudumia. Majusi hawakujua namna ya kuufanya uonekane mwekundu. Lakini walitabiri kwa usahihi kabisa. Somo kwangu lilikuwa kwamba Mungu si mwenye nguvu tu, bali wakutumainika mno.

Ni Ahadi

Baada ya kutafuta kwa moyo wote, Maria alipata tunu yake: kuangukia kwa furaha mikononi mwa baba yake.

Usiogope mambo ya siku za usoni. Kama umetafuta kwa moyo wote na kusalimisha maisha yako kikamilifu kwa Kristo, huna haja ya kuogopa. Mwishowe au mwisho wa maisha yako, utakuwa salama mikononi mwa Yesu. Mikono ya Baba yako wa mbinguni itakukumbatia kwa pendo la milele.

Jipe moyo; inawezekana. Mungu amekuahidi. “ ‘Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.’ ”

Advertisement - RevivalandReformation 300x250

Ministry reserves the right to approve, disapprove, and delete comments at our discretion and will not be able to respond to inquiries about these comments. Please ensure that your words are respectful, courteous, and relevant.

comments powered by Disqus

 

back to top